Date of issue: 27.11.2013
Song language: Swahili
Nitarejea(original) |
Vipi mizigo umeshaweka tayari |
Sijechelewa nkaachwa na gari |
Basi jikaze usilie mpenzi |
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi |
Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna |
Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna |
Roho yangu inauma, sema ntafanya nini na pesa sina |
Nakuonea na huruma, bora niende mjini kusaka tumaa |
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea |
Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea |
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea |
Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea |
Wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi |
Ukumbuke na moyo utajawa na simanzi |
Ntakapokuwa nakwenda shambani afu niko peke yangu honey |
Ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aaah |
Pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani |
Sina wakunitua nyumbani ntaliaa |
Maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo |
Hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo |
Vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh |
We niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh |
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea |
Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea |
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea |
Nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea |
Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi |
Usisahau kama mkeo na wana, umetuacha na dhiki |
Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki |
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki |
Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi |
Kumbuka mkeo na wana nyumbani, umetuacha na dhiki ooh |
Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki |
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki |
Ntarejea mama |
Niombee nirude salama |
Ohhh watoto wadanganye |
Ihh, ohh |
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea |
Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea |
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea |
Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea |
(translation) |
How are you packing? |
It was not long before I was abandoned by a car |
So try not to cry, darling |
I will come back and pray to the Almighty |
The hardships and famines throughout the season are no harvest |
I often feel uncomfortable when you have to chew |
My soul aches, tell me what to do and I have no money |
I feel sorry for you, I better go to the city in search of rest |
If the children cry out to me tell them tomorrow I will come back |
Deceive them with handkerchiefs, tell them I will bring candy |
If the children cry out to me tell them tomorrow I will come back |
And do not grow weary, and pray for me daily |
They know that souls and souls will be anxious |
Remember and the heart will be filled with grief |
When I go to the field afu I am alone honey |
When I come to have neighbors I will hurt aaah |
When I come out of the well or I have wood on my head |
I have no one to take me home and I will cry |
Your words make me feel uncomfortable with thoughts |
Even your partner has never been to this house before |
As I go and I don't know where to sit or dress ooh |
Pray for me to be spared the plague and the disease ooh |
If the children cry out to me tell them tomorrow I will come back |
Deceive them with handkerchiefs, tell them I will bring candy |
If the children cry out to me tell them tomorrow I will come back |
And do not tire of persevering and praying for me every day |
When you leave if you arrive safely, remember us too |
Do not forget if your wife and children, you have left us with stress |
So don't worry but please be very careful, be afraid of friends |
If they cheat you even with sorghum seeds, tell them I will not be deceived |
When you leave if you arrive safely, remember us too |
Remember your wife and sons at home, you have left us with stress ooh |
So don't worry but please be very careful, be afraid of friends |
If they cheat you even with sorghum seeds, tell them I will not be deceived |
I will not return to my mother |
Pray for me to return safely |
Ohhh kids cheat |
Ihh, ohh |
If the children cry out to me tell them tomorrow I will come back |
Deceive them with handkerchiefs, tell them I will bring candy |
If the children cry out to me tell them tomorrow I will come back |
And do not grow weary, and pray for me daily |
Name | Year |
---|---|
Tetema ft. Diamond Platnumz | 2019 |
Darwin's Nightmare ft. Abigoba, Matmon Jazz, Danny Massure | 2015 |
Shu! | 2023 |
Kamata | 2021 |
Kainama ft. Burna Boy, Diamond Platnumz | 2019 |
Jeje | 2020 |
African Beauty ft. Omarion | 2018 |
Gidi | 2022 |
Baikoko ft. Diamond Platnumz | 2021 |
Penzi ft. Diamond Platnumz | 2019 |
Et toi tu crois ft. Hawa, Fouley Badiaga | 2017 |
Yo Pe ft. Diamond Platnumz | 2021 |
IYO ft. Focalistic | 2021 |
Gimmie ft. Rema | 2021 |
Catch a Fire | 2011 |
Inama ft. Fally Ipupa | 2019 |
Love You Die ft. Patoranking | 2017 |
Waah! ft. Koffi Olomide | 2020 |
Katika ft. Diamond Platnumz | 2018 |
Haunisumbui | 2022 |